Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Ezedin Abdel Aziz Khalil, anayefahamika zaidi kama Yasin al-Suri.
Al-Suri ni mwezeshaji wa al-Qa’ida (AQ) aliye na makao yake nchini Irani. Al-Suri amehawilisha pesa na kurutu kutoka kote Mashariki ya Kati hadi Irani, halafu kuendelea hadi Pakistani, kuwaunga mkono viongozi wakuu wa AQ. Mamlaka za Irani zinadumisha uhusiano na al-Suri na zimemruhusu kuendesha shughuli zake ndani ya mipaka ya Irani tangu mwaka 2005. Hapo awali Al-Suri alikamatwa na mamlaka za Irani mnamo mwezi Disemba, mwaka 2011 baada ya tangazo la Tuzo kwa Mahakama kutoa ahadi ya tuzo katika juhudi za kutafuta taarifa kumhusu.
Mnamo tarehe 28 mwezi Julai, mwaka 2011, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja al-Suri kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Suri katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Suri. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa AQ, iliyotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni.
