Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Zerrin Sari, anayejulikana pia kama Fatma Gulten na Hale Melis. Sari ni kiongozi muhimu katika Chama/Umoja wa Kimapinduzi wa Ukombozi wa Watu (DHKP/C), kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni ambalo limeshambulia majengo ya serikali ya Uturuki na wafanyakazi na vilevile majengo ya majeshi na ya kidiplomasia ya Marekani nchini Uturuki tangu miaka ya elfu moja mia tisa na tisini. Lengo la DHKP/C ni kufukuza uwepo wa Marekani na NATO kutoka Uturuki na kuanzisha taifa la kisoshalisti.
Ingawa Sari alifungwa jela kwa shughuli zake, aliachiliwa huru mnamo mwaka 2008 baada ya kifo cha mumewe, Dursun Karatas, mwanachama mwanzilishi wa DHKP/C. Anaaminika kuwa alitekeleza majukumu muhimu katika mashambulio ya mnamo mwezi Machi, mwaka 2013 dhidi ya makao makuu ya Chama cha Haki na Maendeleo (AKP) na Wizara ya Sheria ya Uturuki mjini Ankara, ambayo yalimjeruhi mtu mmoja, na mashambulio ya tarehe 20 mwezi Septemba, mwaka 2013, dhidi ya makao makuu ya polisi wa Uturuki na majengo ya makazi ya polisi mjini Ankara.
