Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa zinazopelekea kufikia wahusika kwenye utekaji nyara wa raia wa Marekani Ihsan Ashour mjini Baghdad mnamo tarehe 13, mwezi Disemba mwaka 2019.
Ashour, ambaye ana uraia wa Marekani na Iraki, alikuwa Iraki kwa shughuli zake za kibinafsi. Alitekwa nyara na wanaume wapatao 10 wenye silaha na waliofunika nyuso zao na kuvalia mavazi meusi katika Wilaya ya al-Sha’ab, karibu na Mji wa Sadr, wakati wa maandamano ya halaiki eneo la Mraba wa Tahrir la mji mkuu. Watekaji wake walimkaba koo, wakampiga, na kushtukiza mwili wake kwa kutumia umeme kabla ya kumwendesha na kuvuka mpaka na kuingia Irani. Nchini Irani, kundi jingine la watekaji nyara lilimhoji Ashour kuhusu madai ya shughuli za kijasusi. Baada ya kuamua kwamba hakuwa jasusi, watekaji nyara wake walimrejesha Ashour Iraki, ambako aliendelea kuteswa na kuhojiwa. Aliachiliwa huru mnamo mwezi Mei, mwaka 2020, na akarejea nyumbani Marekani.
