Khalil Yusif Harb

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Khalil Yusif Harb, anayejulikana pia kama Sayyid Ahmad na Abu Mustafa. Harb ni mshauri wa karibu wa Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO), na ametumika kama mjumbe mkuu wa kijeshi wa kundi hilo nchini Irani na kwa mashirika ya kigaidi ya Kipalestina. Harb ameongoza na kusimamia shughuli za kijeshi za Hizballah kwenye Maeneo ya Palestina na mataifa kadha kote Mashariki ya Kati. Tangu mwaka 2012, Harb amehusika na uhawilishaji wa kiasi kikubwa cha pesa hadi kwa washirika wa kisiasa wa Hizballah nchini Yemeni.

Mnamo tarehe 22 mwezi Agosti, mwaka 2013, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Harb kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Harb katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Harb. Vile vile, ni kosa la jinai kutoa makusudi, au kujaribu kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa FTO Hizballah.

Skip to content