Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Issa Barrey kwa kushiriki kwake katika shambulio la mwaka 2017 la Tongo Tongo, nchini Nijeri. Issa Barrey anaaminika kuwa msaidizi muhimu wa ISIS-Sahara Kuu (ISIS-GS).
Mnamo tarehe 4 mwezi Oktoba, mwaka 2017, karibu na kijiji cha Tongo Tongo, nchini Nijeri, wapiganaji wenye uhusiano na ISIS-GS waliwashambulia wanachama wa kikundi cha Vikosi Maalum vya Marekani waliopewa jukumu la kufunza, kushauri, na kusaidia wanajeshi wa Nijeri kupambana na ugaidi. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Nijeri. Wamarekani wawili zaidi na Wanijeri wanane walijeruhiwa katika tukio hilo. Mnamo tarehe 12 mwezi Januari, mwaka 2018, kiongozi wa ISIS-GS Adnan Abu Walid al-Sahrawi alidai kuhusika na shambulio hilo.
