Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Husayn Muhammed al-Umari, anayejulikana pia kama Hussein Mohammed al-Umari na Abu Ibrahim. Al-Umari anasakwa kwa jukumu lake katika shambulio la bomu la mwaka 1982 dhidi ya Ndege ya Pan Am 830. Al-Umari ni bingwa wa kuunda mabomu na aliwahi kuwa wakati mmoja kiongozi wa Shirika la Mei 15 lililo la kigaidi.
Mnamo tarehe 11 mwezi Agosti, mwaka 1982, bomu, ambalo linaaminika kubuniwa na kujengwa na al-Umari, lililipuka ndani ya Ndege ya Pan Am 830 ikiwa na abiria 267 na wahudumu ikiwa safarini kutoka mji wa Tokyo, Japani, kuelekea Honolulu, Hawaii. Mlipuko huo ulimuua abiria mwenye umri wa miaka 16 na kuwajeruhi wengine 16. Al-Umari na watu wengine wawili walifunguliwa rasmi mashtaka nchini Marekani kuhusiana na shambulio hilo la bomu. Serikali ya Ufaransa pia ilimfungulia rasmi mashtaka al-Umari kwa mashambulio ya bomu ya mwaka 1985 dhidi ya duka la Marks & Spencer na Benki ya Leumi.
Al-Umari ana pasipoti ya Lebanoni na huenda anaishi Iraki au Lebanoni. Yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya FBI. Wizara ya Ulinzi ya Marekani pia inaahidi tuzo ya hadi dola laki mbili kwa taarifa zitakazowezesha kunaswa kwake.
