Mtandao wa Kifedha wa Hizballah

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara | Amerika Kaskazini na Kusini | Asia Kusini na Kati | Asia Mashariki na Pasifiki | Kidunia | Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati | Ulaya na Eurasia

Tuzo

Hadi dola milioni 10

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa zitakazowezesha kuvurugwa kwa taratibu za kifedha za Hizballah. Hizballah hutegemea mitandao ya ufadhili na uwezeshaji ili kudumisha shughuli zake na kutekeleza mashambulio duniani. Hizballah hupata karibu dola bilioni moja kila mwaka kupitia msaada wa moja kwa moja wa kifedha kutoka Irani, biashara na uwekezaji wa kimataifa, mitandao ya wafadhili, ufisadi, na shughuli za utakasishaji pesa.

Hizballah hutumia pesa kufadhili shughuli zake za uovu kote ulimwenguni, ikiwamo; kuwapeleka wapiganaji wake nchini Siria ili kusaidia udikteta wa Assad; shughuli zinazodaiwa za upelelezi na ukusanyaji wa taarifa za kijasusi nchini Marekani; na uimarishaji wa uwezo wa kijeshi kiasi kwamba Hizballah inadai kuwa na makombora yanayoelekezwa kwa usahihi. Shughuli hizi za kigaidi zinafadhiliwa kupitia mtandao wa kimataifa Hizballah wa wafadhili wa kifedha na shughili — wawezeshaji wa kifedha na muundombinu, vitu ambavyo ndivyo uhai wa kundi hilo. Hizballah hupokea kiasi kikubwa cha silaha, mafunzo, na fedha kutoka Irani, nchi iliyotajwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani kama Taifa Linalofadhili Ugaidi.

Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja Hizballah kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu cha 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Baadaye, mnamo tarehe 31 mwezi Oktoba, mwaka 2001, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja Hizballah kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Hizballah katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Hizballah. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani inaahidi kutoa tuzo kwa taarifa zitakazowezesha kutambuliwa na kuvurugwa kwa:

  • Vyanzo vingi vya mapato ya shirika hilo au taratibu zake muhimu za uwezeshaji wa kifedha;
  • Wafadhili wakuu na wawezeshaji wa kifedha wa Hizballah;
  • Taasisi za kifedha na wabadiklishaji pesa ambao kwa makusudi wanawezesha miamala mingi ya Hizballah;
  • Biashara na miradi ya uwekezaji, zote zinazomilikiwa na kudhibitiwa na Hizballah;
  • Kampuni laghai zinazoonekana kama zinafanya biashara halali zinazoshiriki ununuzi wa teknolojia inayoweza kutumiwa kwa malengo ya amani au ya kivita; na
  • Njama za kihalifu zinazohusisha wanachama na waungaji mkono wa Hizballah, ambao wanalinufaisha shirika hilo kifedha.

Skip to content