Hasan Izz-al-Din

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Hasan Izz-al-Din, anayejulikana pia kama Ahmed Garbaya na Samir Salwwan. Izz-al-Din, anayedaiwa kuwa mwanachama wa Hizballah, anasakwa kwa jukumu lake katika utekaji nyara wa Ndege ya TWA 847 mwaka 1985.

Mnamo tarehe 14 mwezi Juni, mwaka 1985, magaidi waliiteka nyara Ndege ya TWA 847 ilipokuwa ikisafiri kutoka Athens kwenda Roma. Kwa zaidi ya siku 17, ndege hiyo iliolazimishwa kutangatanga juu ya Bandari ya Meditereni ikiwa na abiria 153 na wahudumu, kutoka Beirut kwenda Aljias na kurudi tena, ikitua Beiruti mara tatu. Wakati wa kutua kwa kwanza mjini Beirut, watekaji nyara hao walimchapa vibaya, kisha wakampiga risasi na kumuua mpigambizi Robert Stethem wa Jeshi la Wanamaji la Marekani.

Mnamo tarehe 14 mwezi Novemba, mwaka 1985, Izz-al-Din alifunguliwa rasmi mashtaka kwa jukumu lake katika kupanga na kushiriki utekaji nyara huo. Mnamo tarehe 12 mwezi Oktoba, mwaka 2001, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Izz-al-Din kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Izz-al-Din katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Izz-al-Din. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni. Izz-al-Din yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI. Anaaminika kuwa nchini Lebanoni.

Skip to content