Hamad el Khairy

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara | Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Hamad el Khairy, anayejulikana pia kama Amada Ould Kheirou au Abou Qumqum, kwa jukumu lake kama kiongozi mwanzilishi wa kundi la kigaidi la Vuguvugu la Umoja na Jihad Afrika Magharibi (MUJWA).

Chini ya uongozi wa Khairy, wanachama wa MUJWA walitekeleza mashambulio ya kigaidi na utekaji nyara wa wanadiplomasia wa kigeni na watu wengine. Khairy alidai kuhusika na utekaji nyara wa mnamo mwezi Aprili, mwaka 2012 wa wanadiplomasia saba wa Aljeria nchini Mali, na alitokea kwenye video za MUJWA akitoa vitisho dhidi ya wale waliolipinga shirika hilo. Mnamo mwezi Januari, mwaka 2012, Khairy alisema kwamba lengo la MUJWA lilikuwa “kuweka sheria za Kiislamu, sharia, kote Afrika Magharibi.”

Kabla ya kuwa kiongozi katika MUJWA, Khairy alikuwa mwanachama wa al-Qa’ida Kwenye Maghreb ya Kiislamu na alipanga shughuli za kigaidi dhidi ya nchi ya Mauritania. Mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2011, Khairy aliamrisha utekaji nyara wa wafanyakazi wa kutoa msaada watatu kutoka Ulaya nchini Aljeria, wakawajeruhi wawili kwa risasi.

Mnamo tarehe 7 mwezi Disemba, mwaka 2012, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Khairy kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Khairy katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Khairy.

Skip to content