Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni nne kwa taarifa kumhusu Cemil Bayik. Bayik ni Mwanachama wa Kamati ya Utendaji, kiongozi mwandamizi, na mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK), kinachojulikana pia kama Kongra-Gel. PKK ni chama kilichotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO).
Wizara wa Fedha ya Marekani ilimtaja Bayik kama Mlanguzi wa Dawa za Kulenya Mwenye Sifa Maalumu (SDNK) kuambatana na Sheria ya Kutaja Vigogo wa Kigeni wa Dawa za Kulevya (Sheria ya Kigogo) mnamo tarehe 20 mwezi Aprili, mwaka 2011.
