Shambulio Dhidi ya Majengo ya Ubalozi Mdogo wa Muda wa Marekani na Jengo la Dogo lililounganishwa la Marekani

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 10

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa kuhusu shambulio dhidi ya Jengo la Ubalozi wa Muda wa Marekani na Jengo la Dogo lililounganishwa la Marekani mjini Benghazi, nchini Libya. Mnamo tarehe 11 – 12 mwezi Septemba, mwaka 2012, Wamarekani wanne — Balozi wa Marekani nchini Libya John Christopher Stevens, Ofisa wa Utumishi wa Nje wa Usimamizi wa Taarifa, Sean Smith, na Wataalamu wa Usalama wa Kiulinzi Glen Anthony Doherty na Tyrone Snowden Woods— waliuliwa katika shambulio la kigaidi dhidi ya Jengo la Ubalozi wa Muda wa Marekani na Jengo Dogo lililounganishwa la Marekani mjini Benghazi. Magaidi walianzisha msururu wa mashambulio yakihusisha uchomaji moto kwa makusudi, silaha za kiotomatiki, makombora ya kurushwa kwa roketi, na makombora mengine dhidi ya majengo hayo mawili ya Marekani, pamoja na wafanyakazi wa Marekani waliokuwa wakisafiri kati ya maeneo hayo mawili. Aidha, mashambulio hayo yaliwajeruhi vibaya wafanyakazi wengine wawili wa Marekani, yakawajeruhi walinzi watatu wa kandarasi raia wa Libya, na kusababisha uharibifu na kuondokewa kwa majengo yote mawili.

Balozi John Christopher Stevens, mwenye umri wa miaka 52, alizaliwa kaskazini mwa California na alianza kazi yake katika Utumishi wa Nje mnamo mwaka 1991. Balozi Stevens alitumika kwenye vituo vingi vya ng’ambo na ndiye aliyekuwa Kaimu Balozi nchini Libya kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2009. Kuanzia mwezi Machi, mwaka 2011 hadi mwezi Novemba, mwaka 2011, Balozi Stevens alikuwa Mwakilishi Maalumu katika Baraza la Kitaifa la Mpito la Libya, na aliwasili jijini Tripoli mnamo mwezi Mei, mwaka 2012 kama Balozi wa Marekani nchini Libya. Kabla ya kujiunga na Utumishi wa Nje, Balozi Stevens alikuwa mwanasheria wa biashara za kimataifa jijini Washington, D.C. Hapo awali alifundisha Kiingereza kama mfanyakazi wa Shirika la Kujitolea, yaani Peace Corps, nchini Moroko kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1985. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Hillary Rodham Clinton alimtambua Balozi Stevens kama “jasiri na mtu mwema, balozi mkamilifu, na shujaa wa Marekani.”

Sean Smith, mwenye umri wa miaka 34, alizaliwa mjini San Diego, California na akajiunga na Jeshi la Angani mnamo mwaka 1995, akitumika kama mtaalamu wa matengenezo ya redio ya ardhini na Sajini wa Wafanyakazi. Smith alijiunga na Utumishi wa Nje mnamo mwaka 2002 kama Ofisa wa Usimamizi wa Taarifa, akahudumu uhawilishaji mbalimbali ng’ambo ikiwamo Baghdad, Pretoria, Montreal, na The Hague. Smith alisafiri kwenda Benghazi mnamo mwezi Septemba, mwaka 2012 ili kutoa usaidizi wa mawasiliano na usimamizi kwa Jengo la Ubalozi wa Muda wa Marekani.

Glen Anthony Doherty, mwenye umri wa miaka 42, alizaliwa Winchester, Massachusetts na akajiandikisha kama SEAL wa Jeshi la Wanamaji mnamo mwaka 1995, akatumika Iraki na Afuganistani wakati wa kazi yake. Kabla ya kujiunga na Jeshi la Wanamaji, Doherty pia alifanya kazi kama mkufunzi wa kulipwa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu, akaenda chuo cha urubani wa ndege, na alikuwa mkufunzi mwenye uzoefu mwingi wa utabibu wa dharura na urubani. Mnamo mwaka 2005, Doherty alianza kufanya kazi kama ofisa wa ulinzi wa kandarasi, akiwapa ulinzi maofisa wa Wamarekani ng’ambo. Doherty alisafiri kwenda Benghazi mnamo mwezi Septemba, mwaka 2012 ili kutoa ulinzi kwa wafanyakazi wa Marekani.

Tyrone Snowden Woods, 41, alizaliwa Portland, Oregon na alitumika kama SEAL wa Jeshi la Wanamaji kwa miaka ishirini, akizuru mara nyingi kikazi nchini Somalia, Iraki, na Afuganistani. Woods pia alikuwa muuguzi aliyesajiliwa na tabibu wa dharura aliyeidhinishwa. Mnamo mwaka 2010, Woods alianza kufanya kazi kama ofisa wa ulinzi wa kandarasi, akitoa ulinzi kwa maofisa wa Marekani ng’ambo. Alitumika kote duniani akiwalinda maofisa. Woods alisaifiri kwenda Benghazi mnamo mwezi Septemba, mwaka 2012 ili kutoa ulinzi kwa wafanyakazi wa Marekani.

Skip to content