Shirika la Kimapinduzi la 17 Novemba (17N)

Ulaya na Eurasia

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Shirika la Kimapinduzi la 17 Novemba (17N) lilianzishwa mnamo mwaka 1975 kama kundi la mrengo wa kushoto lenye itikadi kali. Kundi hilo lilitaka kuondolewa kwa kambi za Marekani kutoka Ugiriki, kuondolewa kwa majeshi ya Uturuki kutoka Saiprasi, na kukatwa kwa uhusiano kati ya Ugiriki na NATO na Muungano wa Ulaya. 17N ilihusika na matendo mengi ya kigaidi nchini Ugiriki, yakiwamo mashambulio ya kupiga risasi, kwa makombora ya roketi, na ya mabomu ya kutegwa kwenye gari. Kampeni ya kigaidi ya kundi hilo ilisababisha vifo vya wamarekani wanne: William Nordeen, Ronald Stewart, George Tsantes, na Richard Welch. Kundi chipukizi kutoka 17N lilidai kuhusika na shambulio la Ubalozi wa Marekani jijini Athens mnamo tarehe 12 mwezi Januari, mwaka, 2007 kwa makombora ya kurushwa kwa roketi.

Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja 17N kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni (FTO) chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo tarehe 3 mwezi Septemba, mwaka 2015, Wizara ya Mambo ya Nje ilibatilisha kutajwa kwa 17N kama FTO.

Skip to content