Kuhusu
Vuguvugu la Umoja na Jihad Afrika Magharibi (MUJWA) lilitokea Afrika Magharibi mnamo mwaka 2011 baada ya kujitenga kutoka al-Qa’ida katika eneo la Kiislamu la Maghreb. Mnamo mwaka 2013, kundi hilo liliungana na al-Mourabitoun, ambayo baadayelilijumuishwa na Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitaja JNIM kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya Sheria ya Uhamiaji na Uraia (kama ilivyorekebishwa) mnamo tarehe 6, mwezi Septemba, mwaka 2018.
