Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK)

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati | Ulaya na Eurasia

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) ni kundi la Wakurdi wanaotaka kujitenga ambacho kimsingi kinaendesha shughuli zake kaskazini mwa Iraki na kusini-mashariki mwa Uturuki. Kundi hilo, ambalo kimsingi linawajumuisha Wakurdi wa Uturuki, lilizindua kampeni ya matumizi ya nguvu mnamo mwaka 1984. Lengo la awali la PKK lilikuwa kuanzisha taifa huru la Wakurdi kusini-mashariki mwa Uturuki. Mapema miaka ya tisini, PKK ilizidisha shughuli zake kupita uasi uliojikita sehemu za vijijini kushiriki ugaidi wa mijini.

Kundi la PKK lilisitisha matumizi ya nguvu kuanzia mwaka 1999 hadi mwezi Juni mwaka 2004, wakati mrengo wake wa wapiganaji wenye msimamo mkali lilipochukua udhibiti na kubatilisha uamuzi huo wa kusitisha vita kwa hiari. Mnamo mwaka 2009, serikali ya Uturuki na PKK walianzisha tena majadiliano ya amani. Hata hivyo, mazungumzo yalivunjika baada ya PKK kufanya shambulio mnamo mwezi Julai, mwaka 2011, ambalo liliwaua wanajeshi 13 wa Uturuki. Wapiganaji wa PKK na vikosi vya Uturuki walipigana mara kwa mara mnamo mwaka 2011 na 2012, likiwamo shambulio mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2011 ambalo liliwaua wanajeshi 24 wa Uturuki na ambalo lilikuwa tukio baya zaidi kutokea tangu mwaka 1993. Mnamo mwaka 2018, mashambulio mengi yaliripotiwa kufanywa na PKK dhidi ya majeshi ya Uturuki, likiwamo shambulio ambalo PKK ilidai kutekeleza mnamo mwezi Novemba dhidi ya kambi ya kijeshi ya Uturuki ambalo lilisababisha makumi ya majeruhi.

Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja PKK kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Baadaye, mnamo tarehe 31 mwezi Oktoba, mwaka 2001 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja PKK kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya PKK katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na PKK. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa PKK.

Skip to content