Jemaah Islamiya (JI)

Asia Mashariki na Pasifiki

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Jemaah Islamiya (JI) ni kundi la kigaidi lenye makao yake Kusini-mashariki mwaka Asia linalonuia kuanzisha milki ya khalifa kwenye eneo hilo. JI inahusika na mashambulio makubwa ya kigaidi kwenye eneo hilo, likiwamo lile la bomu la mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2002 dhidi ya klabu ya usiku mjini Bali ambalo liliwaua watu zaidi ya 200, lile la bomu la mnamo mwezi Agosti, mwaka 2003 kwenye Hoteli ya Marriott jijini Jakarta ambalo lilisababisha vifo vya watu 12, na shambulio la kujitoa mhanga la mwezi Oktoba, mwaka 2005 mjini Bali ambalo liliwaua watu 26.

Mnamo tarehe 23 mwezi Oktoba, mwaka 2002, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitaja JI kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa na kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya JI katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na JI. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa JI.

Skip to content