Jeshi Jekundu la Japan (JRA)

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati | Ulaya na Eurasia

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Jeshi Jekundu la Japani (JRA) lilianzishwa karibu mwaka 1970 baada ya kujitenga na Ligi ya Kikomunisti ya Kijapani-Kikundi cha Jeshi Jekundu, yaani Japanese Communist League-Red Army Faction. Malengo ya JRA yalikuwa kupindua Serikali na ufalme wa Japani. JRA ilifanya mashambulio mengi kote duniani, likiwamo shambulio la mwaka 1972 kwenye Uwanja wa Ndege wa Lod nchini Israeli ambalo liliwaua watu 26 na kuwajeruhi 80, jaribio la mwaka 1975 kuutwaa Ubalozi wa Marekani jijini Kuala Lumpur, na shambulio la bomu la mwaka 1988 mjini Naples, Italia, dhidi ya Klabu ya USO, lililowaua watu watano. Kiongozi wa kundi hilo alikamatwa mnamo mwaka 2000, na kundi likatangaza mipango ya kufumukana mnamo mwaka 2001.

Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja JRA kuwa Kundi la Kigeni la Kigaidi (FTO) chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 2001, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilibatilisha kutajwa kwa JRA kama Kundi la Kigaidi la Kigeni (FTO).

Skip to content