Kuhusu
Al-Qa’ida Kwenye Eneo la Mito Miwili ya Nile (AQTN) lilikuwa shirika la kigaidi lenye makao yake Sudani na ambalo lilikula njama kushambulia shabaha za Marekani, Magharibi na Sudani. AQTN ilidai kuhusika na mauaji, mwezi Januari mwaka 2008, ya mwanadiplomasia John Granville wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na raia wa Sudani mfanyakazi wa USAID, Abdelrahman Abbas Rahama.
