Al-Qa'ida nchini Iraq (AQI)

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Al-Qa‘ida nchini Iraq (AQI) ilianzishwa mnamo mwaka 2004 na gaidi marehemu Abu Mus‘ab al-Zarqawi, aliyeahidi utii wa kundi lake kwa kiongozi wa al-Qa’ida (AQ) Usama bin Ladin. Mnamo miaka ya tisini, al-Zarqawi alilipanga kundi la kigaidi la al-Tawhid wal-Jihad – shirika lililotangulia lile la AQI — kupinga kuwepo kwa majeshi ya Marekani na ya Magharibi kwenye mataifa ya Kiislamu na uungaji mkono wa Magharibi na kuwapo kwa Israeli. Al-Zarqawi alisafiri Iraq wakati wa Vita ya Uhuru wa Iraki, yaani Operation Iraqi Freedom – uvamizi wa Iraki uliofanywa na muungano wa mataifa zaidi ya 40 yakiongozwa na Marekani – na akaliongoza kundi lake huko dhidi ya majeshi ya Marekani na ya muungano huo hadi kifo chake mnamo mwezi Juni, mwaka 2006. AQI ililenga majeshi ya Muungano na ya Iraki na raia ili kuwashinikiza wageni kuondoka Iraq, kupunguza umaarufu wa Marekani na serikali ya Iraki miongoni mwa raia wa Iraki, na kuwavutia kurutu. Mnamo mwezi Oktoba mwaka 2006, AQI ilijibandika hadharani jina jipya la Taifa la Kiislamu Iraki. Kundi hilo likawa Taifa la Kiislamu Iraki na Syria (ISIS) mnamo mwaka 2013 baada ya kujitenga na AQ.

Mnamo tarehe 17 mwezi Disemba, mwaka 2004, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja AQI (sasa ikujulikana kama ISIS) kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Awali, mnamo tarehe 15 mwezi Oktoba, mwaka 2004, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja AQI kuwa Gaidi wa kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake, mali yote ya ISIS, na maslahi katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na ISIS. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa ISIS.

Skip to content