Kuhusu
Kundi la kigaidi lisilokuwapo sasa la 15 Mei liliundwa mnamo mwaka 1979. Kundi hilo lilinuia kuendeleza nia ya Palestina kwa kuwaua raia wa Israeli na Marekani na kwa kusababisha madhara kwa maslahi ya Israeli na Marekani kote duniani. Kundi hilo la 15 May Organization lilidai kuhusika katika mashambulizi kadha, likiwamo lile la bomu dhidi ya Ndege ya Pan Am 830 la mnamo mwezi Agosti, mwaka 1982, ambalo lilimuua abiria wa umri wa miaka 16 na kuwajeruhi wengine 16.
