Ahmed Iman Ali

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Hadi dola milioni 3

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Ahmed Iman Ali. Ali ini kamanda maarufu wa al-Shabaab, kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO), ambaye ametumika kama kiongozi wa kundi hilo nchini Kenya tangu mwaka 2012. Yeye huelekeza shughuli za kundi hilo dhidi ya Kenya, ambazo zimelenga wanajeshi wa Kenya nchini Somalia ambao ni sehemu ya Majeshi ya Muungano wa Afrika Nchini Somalia (AMISOM). Shambulio moja kama hilo mnamo mwezi Januari, mwaka 2016 kwenye eneo la El Adde, Somalia, lilikitimua kikosi kizima kutoka kambi ya kijeshi na kusababisha vifo vya wanajeshi zaidi ya 140 wa Kenya waliokuwa chini ya AMISOM.

Ali pia anahusika na kasumba ya al-Shabaab inayolenga serikali na raia wa Kenya, kama vile video ya mwezi Julai, mwaka 2017 ambapo aliwatishia Waislamu wanaotumika kwenye vikosi vya usalama vya Kenya. Ali pia ametumika kama msajili wa kurutu wa al-Shabaab, akizingatia vijana maskini jijini Nairobi, na amechangisha pesa kwenye misikiti ili kuunga mkono shughuli za al-Shabaab.

Mnamo tarehe 8 mwezi Machi, mwaka 2018, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Ali kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Ali katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Ali. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu kula njama ya kutoa, msaada wa nyenyo au rasilimali kwa al-Shabaab, Shirika la Kigaidi la Kigeni.

Skip to content