Abdullah Nowbahar

Asia Kusini na Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 2

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni mbili kwa taarifa kumhusu Abdullah Nowbahar. Nowbahar ni mtaalamu wa vilipuzi anayehusishwa na Hezb-e Islami Gulbuddin (HIG) na ni mwanachama wa mtandao wa washambulio wa muundaji mabomu wa HIG, Abdul Saboor. Nowbahar na Saboor walikuwa wahusika muhimu kwenye shambulio la bomu la kutegwa kwa gari la tarehe 18 mwezi Septemba, mwaka 2012 dhidi ya basi lililowabeba wafanyakazi wa kigeni wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul nchini Afuganistani. Mlipuko huo uliwaua watu 12.

Mnamo tarehe 10 mwezi Machi, mwaka 2016, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Nowbahar kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Nowbahar katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Nowbahar.

Skip to content