Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Abdul Rahman Yasin, anayejulikana pia kama Abdul Rahman Said Yasin na Aboud Yasin. Yasin alimsaidia moja kwa moja gaidi mwanzilishi mwamba Ramzi Yousef katika kutekeleza shambulio la bomu la mwezi Februari, mwaka 1993 dhidi ya Majengo ya World Trade Center mjini New York.
Mnamo tarehe 26 mwezi Februari, mwaka 1993, Yasin aliandamana na Yousef hadi kwenye Majengo ya World Trade Center ndani ya lori lililokuwa limejaa vilipuzi, ambalo waliliacha kwenye maegesho ya chini ya ardhi ya hayo Majengo. Vilipolipuka, mlipuko huo uliwaua watu sita, ukawajeruhi wengine zaidi ya 1,000, na ukasababisha uharibifu wa mamia ya mamilioni ya dola. Yasin alitoroka Marekani kwenda Iraki ili kuepuka kunaswa. Kwa kushiriki kwake katika shambulio hilo, Yasin alifunguliwa rasmi mashtaka kwa makosa mbalimbali nchini Marekani.
Yasin alizaliwa Marekani, akahamia Iraki miaka ya sitini, na akarejea Marekani mnamo mwaka 1992. Ana pasipoti ya Marekani. Yupo kwenye Orodha ya FBI ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi.
