Ulipuaji wa Bomu Lililotegwa ndani ya Lori Kituo cha Biashara ya Dunia mwaka 1993
TKM ililipa tuzo ya dola milioni mbili kwa habari zilizopelekea kukamatwa kwa gaidi Mpakistani Ramzi Ahmed Yousef.
Yousef ndiye alikuwa mwanzilishi mwamba was ulipuaji wa bomu la lori kwenye majengo ya biashara ya World Trade Center mjini New York mwaka 1993 uliowaua watu sita na kuwajeruhi wengine zaidi ya elfu moja. Saa chache baada ya mlipuko huo, Yousef alitoroka kwa ndege kwenda Pakistani.

Yousef alitokeza tena nchini Filipino ambako aliendeleza njama changamano ya kigaidi. Yousef alipanga kumuua Baba Mtakatifu John Paul II mnamo tarehe 14 Januari, 1995 wakati wa ziara ya Papa nchini Filipino, na kulipua ndege 12 za Marekani barani Asia siku chache baadaye. Njama yote ilijulikana kama “Oplan Bojinka”, maneno yenye tafsiri katika simo ya Kiarabu kumaanisha “Operesheni Mlipuko” au “Operesheni Mshindo Mkubwa.”
Kabla waweze kutekeleza mpango wao, Yousef na mla njama mwenza Abdul Hakim Ali Hashim Murad walilazimika kukimbia fleti yao mjini Manila mnamo tarehe 6 Januari, 1995 wakati mchanganyiko wa kemikali ulianzisha wingu la moshi uliomwagika nje ya dirisha la fleti. Yousef alimwuliza Murad kurudi kwenye fleti kupata kompyuta ya kupakata na ushahidi ponza mwingine. Lakini aliporudi kwa fleti, Murad alikabiliwa na polisi ambao tayari walikuwa wamekwishafika mahali hapo. Huku akitambua kwamba lazima Murad alikuwa amekamatwa, Yousef alitorokea Pakistani.
Mnamo Februari 1995, kijumbe mtoa habari, baada ya kuona tangazo la TKM kwenye foda ndogo ya njiti za kiberiti na kutiliwa hamasa na uwezekano wa malipo ya tuzo, aliwasiliana na Ubalozi wa Marekani mjini Islamabad, Pakistani, na kutoa habari zilizopelekea Yousef alipokuwa.
Mnamo tarehe 7 Februari 1995, mamlaka ya Pakistani yakisaidiwa na maajenti maalum wa Usalama wa Kidiplomasia wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani walimkamata Yousef na kumrejesha ahukumiwe Marekani kwa mashtaka ya ugaidi.
Kuanzia mwezi Septemba 1996 hadi Januari 1998, Yousef alishtakiwa mahakamani na kupatikana na hatika ya makosa kuhusiana na ugaidi kwenye kesi tatu tofauti. Mnamo tarehe 8 Januari 1998, mahakama ya shirikisho la Marekani ilimhukumu kufungwa maisha na pia miaka 240 gerezani.
Wasilisha Kidokezi
Fanya jukumu lako. Dhamini ulimwengu salama na siku angavu zijazo. Bonyeza kujifunza kuhusu chaguzi za kuripoti vidokezi vya Tuzo kwa Mahakama.
- watekwa nyara/Utekaji nyara
- Korea Kaskazini
- Kuingilia Uchaguzi
