Mauaji ya Wamarekani
TKM ililipa tuzo kwa mtu aliyetoa habari zilizopelekea kukamatwa kwa Mir Aimai Kansi, jambazi aliyepiga risasi na kuua wafanyakazi wawili na kujeruhi wengine watatu wakiwa njiani kwenda kazini makao makuu ya shirika la ujasusi la Marekani (CIA) mnamo tarehe 5 mwezi Januari, 1993.

Kansi alishambulia bila onyo wala uchokozi, kwa kutumia bunduki lake aina ya AK-47 kupiga risasi ndani ya magari yaliyosimama kwenye taa ya barabarani mbele ya makao makuu ya shirika la ujasusi la CIA.
Kansi alitoroka Marekani mara tu baada ya shambulio hilo na alikuwa mtoro mpaka alipokamatwa tarehe 15 Juni, 1997 katika jimbo la Punjab nchini Pakistani. Alirejeshwa Marekani ili kushtakiwa mahakamani.
Mnamo tarehe 10 Novemba, 1997, Kansi alipatikana na baraza la mahakama ya Fairfax, Virginiana, kuwa na hatia ya mauaji ya wafanyakazi hao wawili wa shirika la CIA. Kansi aliadhibiwa kifo mnamo tarehe 14 mwezi Novemba, 2002.
Wasilisha Kidokezi
Fanya jukumu lako. Dhamini ulimwengu salama na siku angavu zijazo. Bonyeza kujifunza kuhusu chaguzi za kuripoti vidokezi vya Tuzo kwa Mahakama.
- watekwa nyara/Utekaji nyara
- Korea Kaskazini
- Kuingilia Uchaguzi
